Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba amefunguka na kumuasa Meja Jenerali, Yakubu Hassan Mohamed ambaye ameapishwa leo Februari 15, 2018 kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Luteni Jenerali Samuel Ndomba amemtaka kiongozi huyo wa jeshi kutofanya kazi kwa kuangalia ukabila au kuwa na upendeleo wowote kwa ndugu, marafiki au imani ya dini yake na kumtaka kuwa kiongozi mwenye kutenda haki.

“Baada ya kuteuliwa tu jana inawezekana marafiki wamesema Mungu atupe nini na sisi tutafaidi hapana wewe si Mnadhimu Mkuu wa marafiki ila ujue wewe ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Wewe ni Muislam kuteuliwa kwako inawezekana Waislam wamesema na sisi tumepata hiyo siyo sahihi kwani wewe si Mnadhimu Mkuu wa Waislam bali wewe ni Mnadhimu Mkuu wa watu wa dini zote, inawezekana Kabila lako watu wa Irangi huko wanasema na sisi Wairangi siku nyingi tulikuwa hatujapata sasa tumepata watatuona na Mahakama Kuu inahamia huko huko sasa angalia hicho wewe si Mnadhimu Mkuu wa wa Irangi bali wewe ni Mnadhimu Mkuu wa Makabila yote hao wote ni wako” alisisitiza Ndomba

Aidha Ndomba aliendelea kumshauri Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na kumweleza kuwa asikubali familia yake ikavaa koti lake lakini pia akamtaka asijikite kwenye kazi moja kwa moja na kuisahau familia yake na kudai hilo litakuwa ni tatizo.

Bashe na Chadema lao moja
Wazazi waonywa kufelisha wanafunzi

Comments

comments