Mwanaharakati na Mkurugenzi wa kampuni ya CZI, Cyprian Musiba amesema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema alichokisema kwenye mkutano wake na waandishi wa habari si cha kweli bali ni mpango maalum uliokuwa umepangwa na chama chake.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kuligeuza suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji kuwa la kisiasa sio sawa.

Amesema kuwa haipaswi suala la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo kujadiliwa kisiasa bali viachwe vyombo vya dola vifanye kazi yake.

“Ni vyema suala hili viachiwe vyombo vya dola, naona Lema anaongea tu na nahisi hajui utaratibu jinsi dola inavyo fanya kazi, si kila kitu lazima ukiweke hadharani, nimemsikia wakati anaongea na vyombo vya habari anailaumu Serikali kwa suala hili, naomba niseme Mo Dewji sio bilionea wa kwanza kutekwa, wapo wengi tu ambao walishatekwa,”amesema Musiba

Video: Zitto aibua maswali tata utekwaji wa Mo Dewji, Maajabu 12 ya Fry-Over Tazara
Chadema kwafukuta, Kubenea, Komu matumbo joto

Comments

comments