Boeing 747-8 VIP ndiyo ndege pekee ya kifahari zaidi inayomilikiwa na familia ya kifalme ya Qatar.

Ndiyo ndege ya kwanza kugharimu dola za kimarekani milioni 380 sawa na bilioni 700 na milioni 266 za kitanzania.

Ndege hii ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya matumizi binafsi ya familia ya kifahari ya kifalme ya Qatar, ina uwezo wa kubeba abiria 100 tu.

Ndani ya ndege hiyo ni kama upo kwenye nyumba ya kifahari, ina ofisi za kifahari, vyumba vya kulala, makabati ya kuwekea vitu mbalimbali, ina sebule na sehemu ya kulia chakula pamoja na kuta zenye picha..

Hii ndiyo ndege pekee na ya kwanza kutengenezwa kwa njia ya pekee na kutumia mabilioni ya fedha tangu kuja kwa wazo la kuwa na ndege ya kifahari kwa familia hiyo ya kifahari

Ni ndege yenye mwendo kasi kuliko kawaida.

Tazama hapa ndege hizo.

Safari za Zanzibar, Dar zasitishwa
Mesut Ozil ajisifia mwenyewe

Comments

comments