Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) linamshikilia kijana mmoja, Adrew Kevera Yono kwa kutuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa baada ya kukutwa chooni katika ukumbi ambao mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unafanyika.

Kijana huyo ambaye baba yake ni miongoni mwa wanagombea nafasi za uongozi katika shirikisho hilo, ameshikwa chooni akiwa na fedha kiasi cha laki tano na amezigawa katika mafungu ya elfu hamsini akiwa tayari kuwapatia baadhi ya wajumbe wa mkutano huo. Tazama hapa

Waziri 'chupuchupu' kutumbuliwa
Video: ‘Zimbabwe’ ya Roma yaweka historia YouTube

Comments

comments