Dar24 Media, na kampuni yake mama ya DataVision International leo Desema 27, 2017 kupitia kampeni yao endelevu ijulikanayo kama ‘’Tuko Pamoja’’ imefanikisha kumsafirisha mtoto Mariam kwenda nchini India kwaajili ya matibabu,

Kampeni ya Tuko Pamoja, Okoa Maisha ya Mariam imelenga kuarifu Umma wakiwemo wadau kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu msichana mdogo mwenye umri wa miaka (16) anayesumbuliwa na ugonjwa kidaktari ujulikanao kama ”Intestinal Obstruction”  na kuwaomba watanzania kwa ujumla kuhusika katika kampeni hiyo kwa kuchangia kwa namna moja au nyingine ili pamoja kuokoa maisha ya mtoto huyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Masoko wa DataVision International,  ambaye pia ni Msemaji wa Dar24, Teddy Ntemi Qirtu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo jijini Dar es salaam ambako alikuwa akiagwa kwaajili ya kwenda India kwa matibabu.

Aidha amewaomba wananchi na wadau kwa ujumla kumchangia mtoto Mariam ili aweze kuendelea na matibabu yake  nchini India mara baada ya jitihada za madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Muhimbili kushindwa kutatua tatizo hilo na kupelekea kumfanyia oparesheni kumi bila mafanikio.

Amesema kuwa gharama za kuratibu shughuli nzima ya matibabu hayo akiwa nchini India ni kiasi cha shilingi milioni 44 za kitanzania.

Hivyo amewaomba wananchi kuungana na Dar24 kupigania maisha ya mtoto huyo kwa kuchangia fedha kupitia M-lipa, tigo pesa, Airtel Money na M-pesa kwa kuandika namba ya kampuni 400700 na kumbukumbu namba 400700 au kupitia akaunti ya benki ya CRDB kwa akaunti namba 0150021209500 jina la akaunti ni Data Vision International – Tuko Pamoja.

Hata hivyo wamechukua nafasi hiyo kuwashukuru wadhamini wao, Serena Hotel, ID Card Solutions, Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola, Kampuni ya MacLeans BeneCIBO, M-
Lipa, Kampuni ya PR ya AMIFAN na OnDemand.

Vile vile, amewashukuru wale ambao tayari wamekwisha wasilisha michango yao kupitia mfumo maalumu wa Mlipa kama ambavyo imeelekezwa na kuwaomba wadau kuendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya Mariam

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017 pasua kichwa
Lissu afanya muujiza, asimama kwa mara ya kwanza