Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa kazi ya polisi si kupiga risasi na kuuwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kazi ya polisi ni kulinda amani ya wananchi.

Amesema kuwa kuzuia maandamano ya vyama vya siasa ni kosa kwani maandamano hayo yapo kikatiba hivyo polisi wanatakiwa kujikita katika kutekeleza majukumu yao ya kulinda amani na si kuwafyatulia risasi wananchi.

“Kitendo cha polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji ni uvunjifu wa katiba na sheria kwasababu huwezi kupiga marufuku kitu ambacho kiko kwenye katiba,”amesema Mtatiro

 

Video: Kuna njama za kutupa kesi ya Akwilina - Mbowe, Ajirusha baharini kina kirefu
Video: Chama hiki sio cha kigaidi, CCM wasitumie mapanga na bunduki- Mbowe