Mtanzania kutoka mkoani Kilimanjaro aliyehitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari, Ilboro, Gracious Fanuel amekuwa mtanzania wa kwanza kuvumbua na kutengeneza roboti la mkono litakalotumiwa na walemavu wa mkono ili kusaidia kuwezesha kufanya shughuli mbalimbali.

Kijana huyo ni  mshindi wa pili katika shindano lililokuwa linaendeshwa na Umoja wa Mataifa (UN) la kusaka vipaji vya wabunifu mbalimbali na kuwapa jukwaa la kuonesha kazi zao kwenye  maonesho ya biashara ya 42 ya sabasaba.

Akizungumza na Dar24 Media mbunifu huyo ametueleza namna roboti hilo linavyofanya kazi ambapo roboti hilo  linaendeshwa na mfumo uliowekwa kwenye simu ya mkononi kuamuru roboti hilo kufanya shughuli mbalimbali.

Tazama video hapa chini kwa kubonyeza link, ili uweze kutazama roboti hilo likiamuriwa kwa kutumia simu ya mkononi na kuitika amria hizo.

Usajili wa Mattéo Guendouzi Olié wavuja
Askari ajiua kwa risasi akielekea lindoni