Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa amewataka wabunge kuweka kando itikadi za vyama vyao ili waweze kujenga Tanzania mpya na yenye kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

Ameyasema hayo mapema hii leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu diplomasia ya uchumi, amesema kuwa ili nchi iweze kupata maendeleo ni lazima kuwepo na maamuzi ya pamoja bila kujali itikadi za vyama.

Amesema kuwa uchaguzi kwa sasa ulishapita kilichobaki kwa sasa ni kuweka nguvu ya pamoja katika kulisukuma gurudumu la maendeleo kwani kama wataendelea kutofautiana kupata maendeleo itakuwa ni ndoto.

“Ni lazima pande zote tusikilizane na kushauriana kwani kila mmoja ni bora kwa wakati wake, tusijione kama tuko bora sana kuliko wengine, maendeleo hayana vyama,”amesema Msigwa.

‘20 Percent alipunguzwa nguvu na watu hawa...’
Wenger ajibebesha Arsenal miaka miwili zaidi