Msanii wa muziki nchini Uganda, Moses Nakintije Ssekibogo maarufu kama ‘Radio’ amepata ajali mbaya ambapo bado anatibiwa kwenye hopsitali ambayo amelazwa nchini humo.

Taarifa kutoka katika uongozi wake imesema kuwa ‘Radio’ bado hajitambui ingawa mpaka sasa ameanza kutingisha vidole.

“Sasa hivi anaweza kutingisha vidole, ingawa madaktari hawataki atoke kwenye comma, sasa kutokana na reaction ya mwili, inaweza ikaleta madhara kulingana na dawa anazotumia, hivyo anahitaji kupumzika,”umesema uongozi wake

Aidha, Wasanii mbali mbali nchini humo wamekuwa wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii, kumuombea aweze kupona haraka.

Hata hivyo, Radio amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Uganda ambapo amekuwa akifanya maonyesho mbalimbali.

Msigwa na wenzake 12 wafikishwa mahakamani
Wanafunzi wachomana visu kwa kubishania dini