Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi  umetinga jijini Dodoma ambapo wasanii hao wameupokea kwa mikono miwili na kusema kuwa mradi huo ni mkombozi kwa kazi wanayoifanya.

Hayo yamesemwa na Afisa Utamaduni jijini Dodoma, Deusidel Kuzenza alipokuwa akizungumza mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa mradi huo jijini Dodoma.

Amesema kuwa mradi huo utawafikia wasanii wengi ambao watanufaika kulingana na kazi zao kwani mradi huo ni mkombozi kwa kazi zao.

“Kuna wasanii mbalimbali katika mradi huu watanufaika, wachoraji, wapiga picha, wakelezaji, yaani huu mradi ni mkombozi kwa wasanii wetu”, Amesema Afisa utamaduni jijini Dodoma Deusidel Kuzenza

 

Mabasi ya mwendokasi 24 kufanya kazi, 58 yaondolewa barabarani
Video; Mavunde apokea kwa furaha mradi wa TACIP jijini Dodoma

Comments

comments