Imeripotiwa kuwa katika mji wa California nchini Marekani, wanandoa Cameron na Janice Hooker walimteka nyara binti mmoja aliyefahamika kwa Coleen Stan.

Binti huyo alitekwa wakati akitoka kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake mara baada ya wanandoa hao kumpa lifti ya gari.

Wawili hao walimtesa na kumfanya mtumwa wa ngono kwa muda wa miaka 7 hadi pale mke alipoona wivu juu ya binti huyo kutumika kingono na mume wake.

Ndipo alipoamua kutoa taarifa polisi juu ya mateka huyo na kuwa shahidi wa kesi hiyo iliyopelekea mume wake kufungwa jela miaka 104, huku mwanamke huyo akiachwa huru.

Tazama Video hapa chini.

Mtemi Ramadhani ajiondoa kugombea Uenyekiti Simba
Fahamu mji hatari kwa maisha ya wanawake

Comments

comments