Kundi la Migos limeendelea kuweka rekodi za kipekee kwenye muziki kupitia albam yao mpya ya Culture II mbapo hivi punde wametoka ‘Kizilipendwa’.

Migos wameachia video ya wimbo wao mpya ‘Walk It Talk It’ waliyomshirikisha mkali anayevunja rekodi za Billboard, Drake.

Katika video hiyo, Migos na Drake wameurudia muonekano wa miaka ya 1970s, muonekano ambao unaakisi kile kilichofanywa na kundi la WCB kupitia wimbo wao ‘Zilipendwa’.

Jammie Foxx amepewa nafasi ya kunogesha video hiyo akiwa kwenye muonekano wa ‘Diamond wa Zilipendwa’ akiwatambulisha Migos kwenye jukwaa.

Culture II ni albam rasmi ya tatu ya Migos iliyoingia sokoni Januari 26 mwaka huu. Studio zilizoipika ni pamoja na Quality Control Music, Motown na Capitol Records.

Promota atabiri Anthony Joshua kupigwa kwa mara ya kwanza
TRA yaagiza biashara zote zilizofungwa zifunguliwe