Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam, Benjamin Sitta amesema kuwa yuko mbioni kujenga kituo cha daladala cha Kawe ili kuwapunguzia usumbufu wananchi wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam katika mkutano wake na wananchi wa eneo hilo, ambapo amesema kuwa kero ya usafiri ambayo imekuwa ikiwakabiri kwa siku nyingi itapatiwa ufumbuzi.

“Tutaweka stendi ya magari ya kisasa, ili iwe suluhisho la tatizo hili, tunatembea halmashauri yote kwaajili ya kutimiza azma ya Rais wetu Dkt. John Magufuli ya kuwajali wanyonge wote,”amesema Sitta

Hata hivyo, ameongeza kuwa halmashauri imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwaajili ya  vikundi mbalimbali vya wajasiliamali na vijana wanaofanya biashara ndogo ndogo ili kuweza kuwakwamua kiuchumi

Video: Fid Q apigia mstari albam yake mpya, atoa siri ya kuachia mbili kwa mpigo
Wakuu wa Wilaya waagizwa kusimamia wakulima Tumbaku

Comments

comments