Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy amedai kuwa msanii Roma Mkatoliki amerekodi wimbo ambao una lugha ya matusi dhidi ya Rais, na kulaani kitendo hicho.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Kessy ambaye alionesha kuumizwa na kitendo cha kuandika na kurekodi nyimbo zenye lugha za kuudhi dhidi ya Mkuu wa nchi alihoji uhuru na demokrasia inayotoa nafasi hiyo.

“Wewe unamtukana Rais wa nchi umekuwa nani? Uhuru gani, demokrasia gani hii. Unaimba wimbo na mtu wa studio anarekodi, ama kweli huu sio utawala… wangeniachia mimi dakika mbili niwaoneshe hawa,” amesikika Kessy.

“Haiwezekani, Mkuu wa nchi anatukanwa. Ukiusikia huo wimbo wa Roma sijui Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu. Haiwezekani mtu anaachia wimbo kama ule halafu unamshabikia tu,” aliongeza.

Kessy alidai vitendo kama hivyo haviwezi kuonekana katika nchi za jirani pamoja na nchi za Uarabuni huku akitaja hatua kali ambazo zingeweza kuchukuliwa katika nchi hizo.

Angalia video kwa habari zaidi:

Sh. bilioni 105 kukamilisha mradi wa upandaji miti
Serikali kupitia upya Sera ya Sekta ya Utalii