Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ameupokea kwa furaha mradi wa TACIP jijini Dodoma kwa kusema kuwa mradi huo ni mkombozi kwa wasanii.

Ameyasema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jijini humo ambapo amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi ili uweze kuwasaidia.

”Kwakweli mradi huu wa TACIP kwa kuja hapa Dodoma, hii ni fursa kubwa sana kwa wasanii wetu hapa jijini  Dodoma, nawasihi wajitokeze kwa wingi sana kwakua huu mradi ni mkombozi, hapa sisi tutatoa ushirikiano kwa kila kitu sababu nawafahamu vizuri na hizi mnaonyesha juhudi za kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kuzalisha nafasi nyingi za ajira”, Amesema Mavunde

Video: Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania watinga Dodoma
Serikali ya Uganda yamjia juu Trump