Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ilala, Augustino Matefu amemshauri Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad kukaa meza moja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili waweze kumaliza tofauti zilizojitokeza siku za hivi karibuni.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa si vyema kwa viongozi wa ngazi za juu kutofautiana hadharani.

Aidha, siku za hivi karibuni, Spika wa bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa wito kwa CAG kupitia vyombo vya habari akimtaka aripoti bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na kamati ya maadili ya bunge, kufuatia tuhuma ya kulidharirisha bunge.

”Mimi nimuombe Prof. Assad aende Dodoma akahojiwe na kamati ya maadili ya bunge kwani Spika ana mamlaka Kikatiba kumuita mtu yeyote na kumhoji kulingana na kosa alilolifanya,”amesema Matefu

DC Njombe awapa neno Wajasiliamali
Polepole amng'ang'ania Prof. Assad

Comments

comments