Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika maeneo ya Korea, huku Marekani na Korea Kaskazini zikijibizana vikali kuhusu matumizi ya silaha za kivita za Nyuklia.

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema kipindi cha Marekani kuwa na subira na Korea Kaskazini kimepita na Marekani inachotaka sasa ni kuhakikisha Korea kuna usalama kwa amani, kupitia mashauriano, lakini pia njia nyingine zozote zinaweza kutumiwa.

“Kumekuwepo na kipindi cha subira, lakini kipindi hicho cha subira kimemalizika.”

Pence amesema hayo alipotembelea katika eneo ambalo haliruhusiwi kuwa na wanajeshi katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini ambapo aliwasili mjini Seoul saa chache baada ya Korea Kaskazini kutekeleza jaribio la kurusha kombora, ambalo halikufanikiwa.

Amesema Marekani kuisaidia Korea Kusini ni ushirikiano thabiti, hivyo ameitahadharisha Korea Kaskazini na kusema haifai kuwa na shaka kuhusu kujitolea kwa Marekani kuwatetea washiriika wake.

Pia, Pence amelishutumu jaribio la karibuni la makombora la Korea Kaskazini na kusema ni uchokozi ambao hawataufumbia macho.

Aidha, Marekani na Korea Kusini zilianzisha mazoezi ya pamoja ya majeshi yake ya wanahewa, kuhakikisha kwamba wanajeshi wake wako tayari kwa tishio lolote kutoka kwa Korea Kaskazini.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema kuwa Marekani inaweza kuishambulia Korea Kaskazini (kuzuia mashambulio ya Korea Kaskazini) ambapo amesema hayo wakati alipofanya ziara eneo hilo lisiloruhusiwa kuwa na wanajeshi.

Video: "Tuliwachapa vizuri Chelsea" - Mourinho
Marekani yaionya Korea Kaskazini, 'Hatutakuwa na uvumilivu zaidi'