Mtayarishaji wa muziki aliyepika ‘hits’ kadhaa, Maneke amesema kuwa amefanya mabadiliko makubwa katika utendaji wake wa kazi na kuachana na zama za awali alizoziita za ujinga za kufanya kazi bure na wasanii.

Maneke ambaye hivi sasa anafanya kazi katika studio za Spice Music zinazomilikiwa na kampuni ya Starline Films iliyoko Mikocheni B jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amerejea kwenye kiwanda cha muziki baada ya mapumziko mafupi ya kusoma ramani ya soko la muziki wa sasa.

Katika mahojiano maalum na Dar24, kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo Ijumaa jioni, Maneke alisema kuwa wakati ule, alifanya kazi nyingi kubwa bure lakini wasanii walipofanikiwa kwa kazi hizo walijigamba kwa kumiliki milioni mia 200 na majumba ya kifahari, huku yeye akibaki mikono mitupu.

“Inakuaje… namfanyia kazi msanii, nahustle (nahangaika), kesho anabrag (anajivuna), bwana nina milioni 200, 500 anapost mijengo wakati mwanangu hata kodi ya kulipa nyumba unakuwa unakosa,” alisema Maneke.

Mtayarishaji huyo ambaye ni baba wa watoto wawili ameeleza jinsi alivyofanya mabadiliko maisha yake pamoja na kazi zake ndani ya studio za Spice Music, na namna alivyoishi enzi alizoziita za ujinga.

Maneke amepika hits kadhaa ikiwa ni pamoja ‘Nataka Kulewa’ ya Diamond Platinumz, ‘My Baby’ ya Quick Rocka na Shaa na nyingine nyingi.

Angalia hapa mahojiano yote:

Serikali yawashusha presha wakulika wa korosho
Bodi ya Filamu yampa Wema ‘hadidu za rejea’ kumtoa kifungoni