Simba ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi katika makundi makundi kifamilia kama ilivyo kwa binadamu, na familia zao huweza kuwa na simba takribani kumi na tano.

Katika maisha yao ya kifamilia hugawana majukumu ambapo chakula hutafutwa na simba jike na awapo mawindoni jukumu la simba dume huwa ni kulinda mipaka yao ambapo simba humiliki eneo kubwa kuanzia mile 10.

Na jambo mojawapo usilofahamu kuhusu simba ni kwamba Simba jike ndiye humpa ishara simba dume kuwa yupo tayari kwa kujamiana, na dume mara tu apewapo ishara hiyo hutimiza matakwa ya jike lake.

Na simba wanaposhiriki tendo hilo wanauwezo wa kujamiana mara 40 kwa siku na kila tendo kudumu kwa sekunde si chini ya 17.

Fahamu mengine kuhusu simba kwa kutazama video hapa chini.

Serikali ya Awamu hii ya Tano inamsimamo kweli- Zitto Kabwe
Video: Bajeti ofisi ya CAG yafyekwa, Waisilamu wahimizwa kutenda mema , umoja