Brigita Magomi, ambaye ni Mama wa Mariam Mwema ameishukuru Kampuni ya DataVision International kwa kugharamia matibabu ya mtoto wake nchini India.

Ametoa shukrani hizo hii leo mara baada kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa (JNIA) uliopo jijini Dar es salaam akitokea nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu mwanae Mariam.

Amesema kuwa Kampuni ya DataVision International imeonyesha mfano mzuri wa kuwahudumia watu wenye matatizo na wasiojiweza, hivyo makampuni mengine yanatakiwa kuiga kazi nzuri zinazofanywa na Kampuni ya DataVision.

“Nawashukuru sana Kampuni ya DataVision kwa kugharamia matibabu ya mwanangu nchini India, Mungu awabariki sana, sina cha kuwapa, lakini ntazidi kuwaombea ili wajaaliwe kingi zaidi, mwanangu ametibiwa na amerudi salama,”amesema Mama Mariam.

Hata hivyo, Magomi ameipongeza na kuishukuru Dar24 Media kwa kuanzisha kampeni ya kumchangia Mariam kwenda kutibiwa nchini India, kwani Media hiyo ndiyo iliyomuibua Mariam kupitia kipindi chake cha ‘Mikasa’

Ashikiliwa na Polisi kwa kughushi nyaraka za Serikali
TFF yatoa ofa kwa mashabiki, kesho kuingia bure shamba la bibi