Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema zoezi la kuwakamata wazururaji limeanza rasmi leo, Aprili 6, 2020 na kwamba watakaokamatwa watapewa adhabu mbalimbali ikiwemo Kusafisha mitaro, Kusafisha barabara, kufyeka nyasi na kulima bustani.

Makonda amesema kama kuna watu walidhani watapelekwa mahabusu na kula Chakula cha bure wasahau kabisa jambo hilo.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa Uzinduzi wa Shoppers Supermarket ya Mlimani City ambapo ameonyesha kufurahishwa na uwekezaji uliofanyika na wazawa jambo lililosaidia zaidi ya Vijana 205 kupata ajira.

Bofya hapa kutazama zaidi

Rais Kenyatta apiga marufuku usafiri Nairobi kupambana na corona
Yanga yapewa ushauri wa bure

Comments

comments