Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amezindua soko la kimataifa la Madini na Vito, ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka kila Mkoa hapa nchini, kuwa na soko la madini.

Makonda amesema kuwa, uzinduzi wa soko hilo utasaidia wananchi kununua Madini na vito mbalimbali, kwa njia halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuzia wananchi na wageni madini na vito bandia.

‘Katika soko hili yatapatikana madini ya aina zote hivyo itawawezesha watu wote kununua kwa uhalali na biola kutapeliwa,amesema Makonda

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kulitumia soko hilo kwakuwa ni halali na linatambulika na Serikali.

LIVE KILIMANJARO: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura
Nitafurahi kama Rais Magufuli ataniteua tena- Mrema