Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la ghorofa tano la mama na mtoto hospitali ya rufaa ya Mwananyamala na kumtaka mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.

RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.

Amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni…, Bofya hapa kutazama.

Watoto 550,388 kupatiwa chanjo Dodoma
Muuguzi wa kiume abaka hospitalini, DED wa Nachigwea amvuruga Magufuli