Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akishirikiana na Kamanda, Lazaro Mambosasa wamefanya ziara kwenye soko la Kariakoo kukagua vitambulisho kwa wamachinga sokoni hapo.

Ambapo amesikitishwa na baadhi ya mambo yanayofanywa na wamachinga wa soko hilo wanaokwenda kinyuma na agizo la Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari leo, June 4, 2019 Makonda amesema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuangalia ni kwa kiasi gani zoezi hilo limefanikiwa na amebainisha mambo kadhaa yakiwemo baadhi ya machinga kutumia vitambulisho feki, wengine kukodisha vitambulisho hivyo kwa shilingi elfu moja kwa siku, huku wengine kubadilishana vitambulisho hivyo siku za ukaguzi.

Kufuatia mambo hayo Makonda ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya wote jijini Dar es salaam kuhakikisha wamachinga wote wanakuwa na vitambulisho hivyo, kama anavyoeleza hapa chini

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 5, 2019
Video: Jinsi Makonda, Mambosasa walivyomtia mbaroni mmiliki wa kitambulisho feki kariakoo