Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kushikamana ili kuweza kutunza mazingira.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitembelea fukwe za Kigamboni na Ocean road ili kuweza kujionea ujenzi wa kingo za fukwe hizo umefikia hatua gani.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya nchi imeharibiwa mazingira hivyo uharibifu huo kusababisha matatizo mbalimbali yakiwemo mafuriko.

“Ndugu zangu niwaombe tushirikiane kutunza mazingira ili tuweze kuepukana na majanga ambayo yanasababishwa na uharibifu huu, ambao kila siku umekuwa ukisababisha matatizo katika jamii yetu,”amesema Samia Suluhu

Magazeti ya Tanzania leo Januari 18, 2018
Dkt. Abbas awataka waandishi kugeukia maendeleo kuliko siasa