Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewaua majambazi watatu mara baada ya majibizano ya risasi yaliyotokea jijini humo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa bado wanawasaka majambazi wengine wawili waliofanikiwa kutoroka.

”Jeshi la polisi limewaua majambazi watatu katika majibizano ya risasi, lakini kuna wengine walifanikiwa kukimbia lakini bado tunawasaka mpaka tuwapate, ni lazima tukomeshe ujambazi katika kanda yetu,”amesema Kamanda Mambosasa

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 28, 2019
Zijue faida za parachichi katika kulinda afya yako