Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa katika kuenzi yale mazuri yaliyoachwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, Watanzania wanatakiwa kudumisha upendo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Dkt. Mengi alipofika kwa ajili ya kuhani msiba, ambapo amesema kuwa upendo na kujali watu wa aina zote ndio kitu alichofanya marehemu enzi za uhai wake.

“Mzee wetu Mengi ametufundisha kutenda wema na usihitaji shukrani, ndio maana tulishuhudia alijitoa kwa vingi bila kuhitaji kurejeshewa chochote,”amesema RC Makonda

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi amefariki usiku wa kuamkia Alhamisi ya Mei 2, Dubai, Falme za Kiarabu, ambapo kwa mujibu wa mwanasheria wa familia, mwili wake utawasili nchini siku ya Jumatatu ya Mei 6, saa 8 mchana.

Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako
Video: Mapya yaibuka kifo cha Mengi, Waziri afichua siri...

Comments

comments