Baadhi ya maeneo nchini Tanzania bado kumekuwa na vitendo vya Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia ambapo Wasichana wengi wamekuwa wakiolewa katika umri mdogo, wengine wakibakwa na wengine kupata ujauzito huku wakiwa bado wanafunzi.

Janga hili ni kubwa lakini bado wasanii wengi wamekuwa wakishindwa kuonyesha mchango wao ili kulitokomeza kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia mashairi ya nyimbo zao, ila kwa ujasiri na uthubutu, mabinti wawili, Nillah na Tannah wameamua KUSEMA na kulizungumzia janga hilo. Wimbo ambao umezalishwa na Tanzania Bora Initiative na Producer Mocco Genius na video kufanywa na Hascana.

Tazama hapa kuona video hii. Okoa mtoto wa kike, okoa jamii.

Polisi anaswa ‘gesti’ na mwanafunzi anayefanya mitihani
Video: SHTUKA! Piga vita dawa za kulevya - KINASA

Comments

comments