Rais wa 32 wa Marekani, Franklin Roosevelt aliwahi kusema, “kwenye siasa, hakuna kinachotokea kama ajali. Ukiona kimetokea kama ajali ujue kilipangwa ila imekuwa ajali tu wewe kukiona wakati  huo.”

Lakini pia mwandishi nguli na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Mmarekani aliyebarikiwa kuishi miaka 93 akayaona mengi, Doug Larson alisema, “badala ya kumpa mwanasiasa ufunguo wa jiji, inaweza kuwa bora zaidi ukibadili kufuli.” Na Winston Churchill, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, yeye akapingana na waliodai siasa ni mchezo mchafu, yeye anaamini, “Siasa sio mchezo bali ni biashara inayohitaji umakini.”

Hakuna jipya kwenye siasa, yote yanayotokea leo yameshasemwa na yamewahi kutokea, ni vile tu tumeamua kutoyafukua na kujisomea kwa sababu “tuna mambo mengi, muda mchache!”

Mwanasiasa ni kama njiwa, kiuhalisia, ni rahisi kumkamata njiwa wa jirani na kuanza kumfuga ukimpa chakula kizuri. Atakuzalishia, atakusikiliza na atakupa furaha uitakayo hata kwa miaka mitatu, lakini akili yake siku zote huwaza nyumbani kwao. Njiwa mgeni huwa na ramani ya kwao chini ya mbawa zake kama Michael Scofield alivyokuwa na ramani ya gereza mgogoni. Ukishindwa kumfanya ajisikie alipo ni nyumbani, ipo siku usiyoijua “atarudi nyumbani.”

Bofya kutazama zaidi hapa chini

Mtuhumiwa mauaji ya watu 49 msikitini afikishwa mahakamani
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 16, 2019