Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa msimamo wake wa kupinga kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli cha kuzuia mchanga wa dhahabu kusafirishwa nje uko pale pale.

Ameyasema hayo mapema hii leo bungeni mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa kuzuia mchanga huo wa dhahabu kusafirishwa kwenda nchi za nje kutaathiri uchumi kwani atakuwa ameenda kinyume na mikataba ya kimataifa.

“Rais Dkt. Magufuli amefanya kitendo ambacho ni kinyume na mikataba ya kimataifa, kwa hiyo hapa tutegemee hasara kubwa na kutengwa na jumuiya ya kimataifa,”amesema Lissu

Wenger ajibebesha Arsenal miaka miwili zaidi
Samia Suluhu kuzindua miradi mkoani Mara