Wakili wa Kujitegema, Leonard Manyama amewataka Watanzania wawe na tabia ya kupenda kulipa kodi ili kuweza kufikia maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na viongozi wa waendesha boda boda wilaya ya Kinondoni ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi.

Amewataka madereva boda boda hao kufuata sheria za usalama barabarani na kuacha kuendesha kwa mazoea, kitu ambacho kimekuwa kikisababisha ajali mbalimbali.

”Hakuna nchi yeyote ambayo raia wake halipi kodi, maendeleo yote yanatokana na ulipaji kodi, lakini pamoja na hayo, nawashauri mfuate sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kutokea,”amesema Wakili Manyama

Video: Mwili wa Mengi ukiwasili: Dar yasimama kwa masaa 3 / Msafara wazongwa na wananchi kila kona
Makamu wa Rais azindua ripoti ya hali ya mazingira nchini

Comments

comments