Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa alilazimika kufanya mabadiliko kwenye Jeshi la Magereza kutokana kutoa fedha ambazo aliagiza kujengwa kwa nyumba za maaskari lakini mpaka sasa hazijajengwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa vyeo kwa wahitimu wa maofisa na Ukaguzi, ambapo ameshangazwa kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya askari magereza lakini hakuna nyumba iliyojengwa.

”Niwaeleze ukweli huwa ninauvumilivu lakini uvumilivu wa kwenye fedha huwa unanishinda, kule Ukonga nilitoa fedha za kujengea nyumba kwa ajili ya maaskari lakini hakuna kinachojengwa, nimemuagiza Kamishna Magereza azifuatilie hizo fedha,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuwapongeza maaskari ambao watakuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu zao ili kuinua morali ya maaskari hao.

Mradi mkubwa wa umeme waanzishwa wilayani Ludewa
Video: Diamond, Rayvanny wapiga magoti, 'Ni kweli tumekosea'