Mapema leo anayejiita mfalme wa bongo fleva akiwa amevalia nguo za kifalme, Alikiba ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la Dodo akiwa ameshirikisha mwanamitindo Hamis Mobetto akiwa kama dodo malkia kwenye video hiyo.

Alikiba amevunja ukimywa kwa muda mrefu baada ya kukaa kimya bila kuachia ngoma kama ilivyokawaida yake kulinganisha na mpinzani wake Diamond Platinumz ambae amekuwa akiachia ngoma baada ya ngoma.

Aidha ngoma ya Dodo bado tunaitazamia kuvunja rekodi ya ngoma ya ”Seduce me” iliyotazamwa mara milioni moja ndani ya masaa 24 na kushika namba moja kwenye ngoma zilizokuwa zinatrendi katika mitandao ya kijamii wa Youtube.

Tazama hapa na sikiliza kisha shusha komenti zako, ni asilimia ngapi unaweza kumpa Alikiba kwa kuachia ngoma hiyo licha ya kimya kirefu kukaa bila ya kuachia ngoma yeyote, Je amewatendea haki mashabiki?

Jana Aprili 7, 2020 muda wa saa 3 kamili, King Kiba alikuwa mubashara kupitia ukurasa wake wa Instagram akipiga stori mbalimbali kuhusu muziki wake tangu alipoanza hadi aliposasa ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wale waote waliokuwa nyuma ya muziki wa Bongo Fleva kukuwa na kuufikisha ulipo sasa.

Huku akimtaja msanii Ambwene Yessaya maarufu kama AY kuwa ndiye shabiki wake nambari moja aliyemfanya aingie katika muziki na kusema kuwa alipoanza muziki alikuwa anaimba HipPop na baadae aliamua kuachana na HipPop na kuimba nyimbo za R&B ambazo zimemtoa hadi saa na kumfanya aitwe mfalme na mkongwe wa hii gemu ya bongo fleva.

 

BSS waagizwa kulipa milioni 50
LIVE Bungeni: Makadirio bajeti ya TAMISEMI 2020/2021