Wakili wa Kujitegemea, Leonard Manyama amesema kuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kazi yake kubwa ni kukagua matumizi ya ofisi mbambali za serikali.

Akizumgumzia kauli ya CAG aliyoitoa kuhusu bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Manyama amesema kuwa kauli hiyo ni tata na ni tuhuma nzito kwa bunge na inaweza kupelekea madhara makubwa.

“Sisi taifa letu ni la Kidemokrasia, linaheshimu mgawanyiko wa madaraka, tuna Mahakama, tuna Bunge na tuna serikali kuu, mihimili hii kila mmoja unafanya kazi zake huru bila kuingiliwa na mwingine, kwa hiyo matamshi ya CAG akiwa nje ya nchi katika jumuiya za kimaitaifa kwakweli hayakuwa na afya kwa taifa letu,”amesema Manyama

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 14, 2019
Video: Zitto amvimbia Spika kuhusu CAG, sasa kumburuza Mahakamani

Comments

comments