Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa kamwe jeshi hilo haliwezi kufanyakazi zake kwa kuburuzwa na fikra za mtu.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa jeshi hilo linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zilizopo.

Akizungumza kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema kuwa, Mbowe amekuwa na tabia ya kutoa matamko ya mara kwa mara, ikiwemo kauli ya kulituhumu jeshi hilo kuhusika na mauaji ya kiongozi wa Chadema aliyekutwa amefariki dunia katika fukwe za Coco beach.

“Hatuwezi kumuacha mtu atoa kauli ambazo zina utata, kama yeye anajua kile ambacho kimetokea basi lazima atueleze na sisi, anatakiwa awe ni mmoja wa watu watakao tusaidia katika kufanikisha upelelezi wa tukio hilo,”amesema Kamanda Muliro

Video: Jeshi la Polisi lawatoa hofu wananchi kuhusu uchaguzi
Young Africans yaikandamiza Majimaji FC uwanja wa Taifa

Comments

comments