Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa Jeshi la polisi linaendelea na mchakato wa kumtafuta mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ aliyetekwa siku ya Alhamis Oktoba 11,2018 jijini Dar es slaam.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi ili kusaidia kutoa ushirikiano wakati wakiendelea kuwasaka watu wote waliohusika na tukio la utekaji ikiwemo kumpata Dewji mwenyewe.

”Niwahakikishie Watanzania, jeshi la polisi linaendelea kushughulikia tukio la kutekwa kwa Mohamedi Dewji, likiwasaka waliomteka na tutahakikisha wanapatikana, ambapo hadi sasa navyozungumza takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano,” amesema Kangi.

Aidha, Lugola pia amemtaka, IGP Simon Sirro kutoa maelekezo kwa askari wake, kuwaachia ndani ya saa 24 watu wanaowashikilia kwa uchunguzi kuhusiana na kutekwa kwa Mohammed Dewji mara baada ya kuwahoji na kubaini hawahusiki au hawana taarifa kamili.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 14, 2018
Maandalizi ya tamasha la vyakula vya asili lakamilika

Comments

comments