Kitengo cha Utafiti na Data katika Kampuni ya DataVision International, kimeweka kambi katika mikoa 26 ya Tanzania bara, wilaya 181 katika vijiji zaidi ya 4800 kufanya utafiti katika Wizara ya maji, upande wa ubora wa bomba za maji wanazozitumia wananchi.

Katika utafiti huo, tayari watafiti zaidi ya 120 ambao wamesha fanyiwa mafunzo wameanza kukusanya taarifa ambazo zinakusanywa kwa njia ya teknolojia kwa kutumia mfumo wa TIKITI ambao watafiti wana andika takwimu kwa njia ya kisasa zaidi.

Aidha, licha ya changamoto mbalimbali kama hali ya hewa na usafiri, kampuni ya DataVision International imeahidi kukusanya takwimu zilizo na ubora na zitakazo saidia Serikali katika kutoa huduma za maji kwa wananchi kwa ubora zaidi.

Serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyuo vikuu vyote nchini
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 24, 2018