Kampuni ya Airtel imezindua huduma mpya ya ‘TAMBA MITANDAO YOTE’ kwa lengo la kuwapa wateja wake uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wote hata kama mteja hajajiunga na bando.

Huduma hiyo imezinduliwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel, Isaack Nchunda, ambapo amesema kuwa huduma hiyo ya ‘TAMBA MITANDAO YOTE’ inawapa wateja wa Airtel uhakika wa kupiga simu mitandao yote.

”Tunayo furaha kubwa kuzindua huduma hii ambayo inawapa wateja wa Airtel kupiga simu kwenda mtandao wowote hapa nchini kwa gharama nafuu kabisa, hivyo huduma hii itapunguza malalamiko kwa wateja,”amesema Nchunda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano amesema kuwa kulingana na taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) idadi wa watumiaji wa simu za mikiononi imeongezeka.

Habari Picha: JPM aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi
Lissu atangaza tarehe ya kurejea Tanzania, mapokezi yake

Comments

comments