Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, vilivyokuwa vinatumika kabla ya mifuko kuunganisha viendelee kutumika kwa kila mfuko hadi mwaka 2023.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kujadili kwa pamoja kuhusiana na mjadala wa kikokotoo kipya cha mafao kwa wastaafu.

“Formula nzuri ni zile zinazo wapromote wafanyakazi, ndio ninazozitaka mimi, formula zinazowanyima haki wafanyakazi sio formula nzuri, ninashukuru katika kipindi hiki kifupi cha kuunganisha mifuko tumeanza kuona matokeo,”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, hivi karibuni uliibuka mjadala huo baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kutoa kikokotoo kipya ambacho kilikuwa kikitaka mstaafu wa sekta ya Umma kupatiwa asilimia 25 ya mafao yake kwa mkupuo badala ya ile 50 ya mwanzo.

 

 

Rais Magufuli ni Nyerere kwa maneno na matendo – Waziri Hasunga
Maafisa wa Indonesia waonya kuhusu mlipuko wa Volcano