Penzi linapokuwa maarufu inaleta raha, lakini shubiri ni pale ambapo wapenzi hao wanapofikia hatua ya kufarakana na kila mmoja kupita njia yake.

Juz na Vanessa ni moja ya ”Couple” iliyokuwa maarufu na iliyopendwa na watu wengi, wawili hao walipogombana wengi walidhani Vanessa anaweza kuwa katika wakati mgumu kuliko Jux ambaye mapema aliweka wazi juu ya mahusiano yake mapya na mpenzi wake raia wa China aliyefahamika kwa jina la Nnayanka.

Huku Vanessa akisikilizia mashambulizi ambayo Jux amekuwa akiyafanya katika mitandao ya kijamii akirusha picha mbalimbali zikimuonesha akiwa katika viwanja kadha wa kadha vya dunia akila raha na mpenzi wake huyo.

Wawili hao ni kama wapo kwenye vita kali inayowafanya mashabiki wabaki midomo wazi na kuona pambano kama ngoma droo, kwani huku Jux na mchina, huku Vanessa na star wa Marekani, Rotimi  raia wa Nigeria ni mtangazaji lakini pia mcheza filamu Marekani, moja ya kazi yake kali ambayo amefanya vizuri ni tamthilia ya ”Power” ambayo alicheza kama kijakazi wa moja ya tajiri katika tamthilia hiyo.

Ona walichopost leo Vanessa na Rotimi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 30, 2019
Muna: kila wiki ni lazima kwa mganga, bila mganga maisha hayaendi

Comments

comments