Leo Machi 25, 2019 Rais Magufuli amekutana na timu ya Taifa mara baada ya ushindi wa kishindo walioupata kwenye mechi iliyochezwa jana ya  kufuzu michuano ya Afcon kwa kuilaza kifo cha mende timu ya Uganda kwa kuwafunga mabao 3 kwa bila.

Rais Magufuli katika hotuba yake leo alipowaita taifa stars na mpiganaji, Hassan Mwakinyo Ikulu kwa ajili ya chakula cha pamoja amesema kuwa amepita kwenye mitandao ya kijamii ameona namna ambavyo watanzania wamefurahia ushindi huo na kuomba leo kuwa siku ya mapumziko.

Rais Magufuli amesema ”Sikushangaa kuona wengine wamelewa ndio furaha na Watanzania wanapenda furaha” Rais Magufuli.

“Wengine walikuwa wanasema kwanini usitangaze kesho ikawa mapumziko, nikasema Watanzania na mapumziko jamani, ila sikushangaa ndiyo dhana ya kufurahi” Rais Magufuli.

Aidha, ushindi huu umetoa heshima kubwa na kuandika Historia kwa nchi ya Tanzania baada ya kipindi kirefu walipofanikiwa kufuzu mashindano haya.

Hivyo mwaka huu Tanzania imedhamiria na kuahidi kuwa ni zamu zetu.

Video: Tacip yawamulika mafundi majeneza Manzese
Cardi B amburuza mwandishi mahakamani

Comments

comments