Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu suala zima la uhalifu wa makosa ya mitandao ambapo kwa sasa limeshika kasi kubwa

“Chochote kinachofanyika ambacho ni kosa la jinai nawaomba msiende Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa watoa huduma wa mitandao ya simu mbalimbali wala katika vyombo vya kutolea habari bali unapaswa uje katika kituo cha polisi utoe taarifa zako kama ni kosa la jinai, kwa sababu mkienda huko uchunguzi utakuwa shida kwa maana wewe mwenyewe utaweza kusababisha hata yule aliyekutenda uhalifu atoroke,”amesema Mwakalukwa

Video: Polisi Dar wapiga marufuku maandamano ya kufanya maombi
Conte aitabiria Arsenal ubingwa