Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa yeye ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ameteuliwa na Rais Dkt. Magufuli kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Ameyasema Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa mwanasiasa  yeyote duniani hufanya harakati zake kwa lengo la kutaka kupata fursa ya kuingia serikalini na kuwatumikia wananchi.

Akizungumza kuhusu kukihama chama cha ACT- Wazalendo, amesema kuwa utengano wowote ambao hutokea huwa umeambatana na maumivu, hivyo wakati anahama chama hicho wanachama wenzake walimhoji.

“Ili uweze kuingia serikalini lazima utafute njia ambayo itafanikisha kukufikisha, hao wanasiasa wote wanaoandamana na kupiga kelele, lengo lao ni moja tu, ni kutaka kuingia serikalini,”amesema Prof. Kitila Mkumbo

 

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ufaransa
Bilionea Dkt. Shika sasa kuwanyoosha, mabilioni yatua nchini