Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezindua Jengo la Upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala lenye thamani ya Shil. Millioni 420 ambalo litasaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.
 
Jengo hilo la kisasa lenye Ghorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE Kama sehemu ya kuenzi jitihada zake za kuboresha Sekta ya Afya.
 
Amesema kuwa kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto, lakini kupitia jengo hilo vifo vinaenda kupungua.
 
Hata hivyo, Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa 

Tido Mhando kizimbani kwa uhujumu uchumi na mengine
Mbowe, Lowassa kumnadi Salum Mwalimu kesho