Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia wawekezaji wa viwanda vya kuchakata mazao mazao ya mifugo nchini kuwa hakuna mtu yeyote atakayechezea soko la bidhaa hizo kwani Serikali iko macho wakati wote kudhibiti uingizaji holela wa mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi.

Hivyo amesititiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti utoroshaji wa mifugo nje ya nchi na kudhibiti uingizaji holela wa bidhaa za nyama na maziwa hazikulenga kumuonea mtu bali kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji wa viwanda hivyo kuwekeza nchini.

Mpina amesema kuanza kwa viwanda hivyo vipya ni uthibitisho kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini baada ya wawekezaji wengi siku za nyuma kulazimika kufunga viwanda vyao na kukimbia kutokana na utitiri wa bidhaa zilizoingia nchini kwa njia za panya na kutokuwepo ushindani ulio sawa kwenye biashara.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 13, 2019
Nguvu ya upendo wa mama, ilivyokuwa uhai wangu

Comments

comments