Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na watu wa Interpol nchini Kenya, linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini ni namna gani, Raphael Ongangi alitekwa na kufikishwa Mombasa.

Amesema kuwa, wanaendelea na uchunguzi huo kwa kuwa hata taarifa zilizotolewa hapo awali zilitolewa kwa mashaka, ambapo ameongeza kuwa miaka 2 iliyopita, mtoa taarifa ameshawahi kutoa taarifa za uzushi kwamba anataka kutekwa.

”Mtekaji akuteke Tanzania akuchukue hadi Mombasa, tena karibu na nyumba ya shangazi yako!, bila shaka huyo mtu atakuwa anakupeleka nyumbani. Sasa hatuelewi chanzo cha habari hii, na tutakapohakikisha pengine taarifa hizi zilikuwa za kutengeneza mhusika naye atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,”amesema Mambosasa

Raphael Ongangi ambaye ni mfanyabiashara raia wa Kenya alitekwa Juni 24, na kupatikana Mombasa, karibu na nyumbani kwa shangazi yake Julai 2, 2019.

Jogoo aburuzwa mahakamani kwa kuwakera majirani
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2019