Msanii wa nyimbo za Bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money bado anaendelea kufanya vizuri katika sanaa ya muziki na tayari ameachia kazi yake mpya inayofanya vizuri.

Ambapo kabla ya kuingia kwenye fani hiyo Gigy alikuwa mpendezesha video yaani ‘video vixin’ za wanamuziki mbalimbali nchini.

Moja ya nyimbo aliyowahi kuipendezesha ni nyimbo ya msanii nguli nchini, Duly sykes akiwa amemshirikisha msanii chipukizi Harmonize wimbo ujulikanao kama Inde.

Gigy alipoingia kwenye fani ya muziki amefanya nyimbo kadhaa wa kadha lakini wimbo uliomtambulisha vizuri na kukubalika zaidi na wasikilizaji na mashabiki wake.

Ubunifu wa mashairi ya wimbo wa Papa umempa Gigy kiki na kumfanya afanye vizuri katika wimbo huo kwani ni wimbo ulioleta tafsiri mbalimbali kwa mashabiki wake.

Gigy ameachia wimbo wake mpya aliouita Mimina.Kuitazama video hiyo bonyeza link hapa chini

 

Necta yatangaza matokeo kidato cha nne
Mtoto wa miezi nane abakwa, jiji lagubikwa majonzi