Tajiri wa Mashairi na Flow, Fid Q ambaye leo anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa akiachia video na nyimbo mbili kama zawadi kwa mashabiki wake ameeleza siri ya kutoa zote kwa mpigo.

Ngosha ameiambia Dar24 kuwa huu ni wakati ambao mashabiki wake wanaelewa kwa haraka zaidi kuliko wakati mwingine uliopita na kwamba wanavyozidi kuelewa ndivyo atakavyoendelea kuongeza idadi ya ngoma anazotoa kwa mpigo.

Rapa huyo pia amepigia mstari mpango wa kuachia albam yake mpya ambayo amedai itazibeba pia nyimbo zake mbili alizoachia kwa mpigo leo, ‘Ulimi Mbili’ na ‘Fresh’.

Amezungumzia pia kiasi cha kiu ya mashabiki wake akilinganisha na nyimbo alizoziachia leo pamoja na maana yake kwenye muziki.

Angalia video hii kuyapata kiundani mahojiano ya Dar24 na Ngosha:

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 14, 2017
Video: Meya wa Kinondoni kujenga stendi ya Daladala Kawe

Comments

comments