Ukistaajabu ya Musa utaona ya Filauni, huku Indonesia kuna utamaduni unaofahamika kama Ma nene ni utamaduni ambao wafiwa huishi na maiti kwa kipindi cha muda fulani na ndani ya kipindi hiko huwahudumia maiti hizo kama wagonjwa kwa kuwalisha, kuwavisha, kuwaogesha na kuwapa au kuwafanyia marehemu kitu ambacho alikuwa anapenda kukifanya enzi za uhai wake.

Kufanyika kwa utamduni huu ni ishara ya wazi ya kuonesha hisia zao za upendo za kutotaka kuwapoteza wapendwa wao waliotangulia mbele za haki.

Utamaduni wa Manene unafanywa na watu waishio kisiwa cha Sulewasi huko Indonesia na watu hao hufahamika kama Torajan.

Watu hawa wanaamini kuwa kifo sio mwisho wa maisha ya binadamu bali ni hatua nyingine ya maisha ambayo binadamu huipitia.

Utamaduni huu umekuwa kivutio kikubwa kwa wageni toka mataifa mengine ambao hutembelea Indonesia kuona namna binadamu wanavyoishi na kuwahudumia maiti zao ambazo huishi nazo kwa kipindi cha muda mrefu kabla ya kuzizika.

Tazama video hapa chini.

Wasukumwa ndani kwa tuhuma za kula hadharani wakati wa mfungo
DAWASA yaanza zoezi la usajili wa utoaji vibali

Comments

comments