Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa serikali haiwabagui wabunge wa upinzani katika suala la matibabu.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Luninga ya Cloudstv.

Amesema kuwa suala la fedha za matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu lilishashughulikiwa hivyo kuna baadhi ya taratibu ambazo hazikufuatwa.

“Unajua kuna baadhi ya wabunge wanapotosha kwa makusudi suala hili la matibabu, na utaratibu unajulikana kwa kila mmoja, suala hili wamelibadili kuwa la kisiasa, kitu ambacho sio kizuri,”amesema Dkt. Tulia

 

 

Mwadui FC kugangamala kwa Mnyama Leo?

Comments

comments